top of page
WhatsApp Image 2025-10-15 at 20.03.03.jpeg

​Poetry and storytelling empower young people.


At APAO Village, we use words as seeds, poems to inspire, stories to teach, and culture to guide. Through the Malenga wa APAO mentorship, young voices learn to cherish their roots, protect the environment, and carry the vision of APAO Village and SERA2030 into the future.

PART 1: inspiring unit & PEACE during & AFTER election

1. Shukrani kwa Mungu

Mwenyezi Mungu muumba, uliiumba duniaa,

Nchi safi Tanzania, sisi ulitupangia,

Tangu kizazi cha kwanza, hadi kwa mama Samiaa,

Umetupa utulivu, Baba tunakushukuru.

 

Kutoka uhuru wetu, bendera kupaa juu,

Mito, milima na watu, vyote viliwekwa juu,

Ili wote tuabudu, bila vita wala chungu,

Tunakuomba ee Baba, uilinde nchi yetu.

 

Kila kampaini zikija, sisi wote twashiriki,

Kwa haki kupiga kura, tukikumbuka amani,

Umoja wetu imara, tusifate interneti,

Baba utulinde sote, tufikie huko salama.

 

Mwingi twaomba upendo, umwagwe kwa kila mtu,

Chama changu kiwe chako, visituletee gubu,

Tuishi kama watoto, tuijenge nchi yetu,

Mungu tushike mkono, tufike huko salama.

 

Malenga naomba sana, kutoka huku APAO,

Tusiombe kusigana, kama tuwasikiao,

Hata wakati wa kura, hatutaki marumbano,

Mungu tushike mkono, tufike huko salama.

2. Amani ni Tunu

Amani hazina pekee, twaweza kuipoteza,

Kwa matusi na vijembe, twaweza kuyumbishana,

Naomba tushikamane, tujenge hili taifa

Tanzania tuipendee, iwe tulivu daima.

 

Kura ni silaha yetu, lakini siyo ya vita,

Chaguo lako ni letu, kura inatuongozaa,

Tusije kumwaga damu, bali tuwe wa kujenga,

Mshikamano udumu, amani yetu ni tunu.

 

Vyama vipo tofauti, lakini sisi ni ndugu,

Leo tupo jukwaani, kesho twakaa kindugu,

Watoto wapo nyumbani, tusiwatie machungu,

Tulinde yetu amani, amani yetu ni tunu.

 

Viongozi washindapo, tuwape zao heshima,

Tuwaalike APAO, wafike kupumzika,

Ndiyo demokrasia, wote tunayoipenda,

Tuzidi kushikamana, kama taifa thabiti.

 

Amani twashikilia, maendeleo yasonge,

Elimu, afya kinga, uchumi uimarike,

Hatutaki kugombana, kisa kura ziko chache,

Tanzania itasonga, malenga ninatabili.

3. Kura ni Haki


Kura yako ni sauti, usiiuze kwa fedha,
Kwa kikombe cha sukari, wala kipande cha kanga,
Chagua kwa umakini, yule mwenye sera bora,
Tanzania ni urithi, malenga nawakubusha.


Kura ya mtu mmoja, yawaamulia wengi,
Kwa hiyo twende pamoja, ni jukumu la kizazi,
Ukichagua kwa hila, nchi itapata ganzi,
Tusiuze kura zetu, malenga nawakubusha.


Tusipochagua vyema,  baadaye tutajutia,
Maendeleo kukwama, uchumi kusuasua,
Marumbano kutawala, mashimo kwa barabara,
Kura yako ni hazina, malenga nawakubusha.


Chama changu au chako, vyote vya watanzania,
Uchaguzi siyo mwisho, maisha yaendelea,
Tusikubali michongo, waje kutuchonganisha,
Kura ya haki  Suluhu, tujenge mshikamano.


Wote tukipiga kura, kwa heshima na upendo,
Taifa letu lapona, tutashinda changamoto
Tanzania ya wapendwa, tutaifanya mfano,
Kura ya haki  Suluhu, tujenge mshikamano.

4. Umoja Wetu


Tanzania ya amani, umoja wetu thamani,
Mshikamano makini, tuliuanza zamanii,
Kila chama ni makini, kikijali masirahi,
Umoja ndio Suruhu, ya kushinda kila vita.


Jukwaani twasikia, sauti  zikingurumaa,
Mwisho wa yote taifa, ni moja la kulijenga,
Tusipoteze hekima, tusiuvunje umoja,
Tanzania mbele sana, umoja ndiyo Suruhu.


Wapinzani-watawala, sisi wote twawapenda,
Mshindi twakaribisha, bule APAO kulala,
Siasa zikishapita, kazi kubwa ni maisha,
Tanzania mbele sana, umoja ndiyo Suruhu.


Tukiwa wamoja sana, tutashinda changamoto,
Kila kitu kiwe bora, mpaka kule makambako,
Yote tuliyoyajenga, yawe daraja la kesho,
Umoja wetu wa dhati, ndiyo amani ya kesho.


Umoja ni neno fupi, maana yake ni pana,
Kushikamana kwa thati, sio jambo la kubeza,
Kugawanyika hatari, kwa tofauti za vyama,
Tanzania yetu moja, tulinde umoja wake.

5. Vijana Wana Nguvu


Vijana ndilo taifa, nguvu ya kesho imara,
Kwa kura mlizoshika, mwelekeo mwaamua,
Msije macho kufumba, mkaipoteza dira,
Mshiriki kwa hekima, Taifa tukalijengee.


Sauti yenu ni kura, thamani yenu twajua,
Msitumike vibaya, kesho mtakuja juta,
Kwa usahihi chagua, uzalendo shikilia,
Tanzania kikinuka, vijana mtapoteza.


Msiwe chombo-vurugu, wala silaha-ghasia,
Jenga imani ya Mungu, tuvuke wote pamoja,
Kwa upendo wa kindugu, taifa litainuka,
Vijana hazina kuu, kwa hili taifa letu.


Shirikishaneni mawazo, bila kujali ya chama,
Kila kijana ni nguzo, ya kulijenga taifa,
Msidanganyike mwanzo, mwisho hesabu twatoa,
Mnaposhiriki kura, Tanzania iwe mbelee.


Vijana mkisimama, taifa letu imara,
Mshikamano twataka, kila kijana changia,
Kila kijana na zaka, taifa kuliombea,
Nguvu zote za vijana, msingi wa Tanzania.

Sustainability

Sustainability

Moringa
bottom of page